Jumanne , 21st Feb , 2017

Serikali imeagiza hospitali zote za mikoa nchini zianzishe kliniki maalum ya kutoa huduma za matibabu ya watumiaji wa dawa za kulevya kwa kutumia methadone, ndani ya miezi sita.

Dkt Kigwangalla katika ziara yake, Mwananyamala

 

Agizo hilo limetolewa na Naibu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla alipotembelea kituo cha kuwahudumia watu wanaotibiwa kuacha dawa za kulevya kwa kutumia methadone kilichopo Hospitali ya Mwananyamala na kumuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya kuhakikisha kuwa kuna Daktari Bingwa wa Afya ya Akili kwenye kila mkoa ili kuanzisha na kusimamia vituo hivyo.

Dkt. Kigwangalla amesema kumekuwepo na ongezeko kubwa la watu wanaohitaji huduma hiyo kwa siku za hivi karibuni kutokana na kuongezeka kwa udhibiti wa dawa za kulevya, huku kukiwapo kwa taarifa kwamba wauzaji wa dawa za kulevya wameathiriwa kwa kupoteza mapato ya shilingi bilioni 70.

Pamoja na mambo mengine Dkt. Kigwangalla amekemea baadhi ya viongozi wanaopotosha jamii kuhusu dawa hizo methadone.

Kwa upande wake muangalizi wa kituo hicho Dkt. Kasian Ndindindi amesema uwepo wa kituo hicho cha Mwananyamala kwa sasa umesaidia kuwahudumia waathirika wa dawa za kulevya 3,351.

Nao baadhi ya watu wanaopatiwa huduma katika kituo hicho wamesema tangu waanze kutumia dawa hizo wamekuwa na unafuu mkubwa