Jumanne , 26th Sep , 2017

Vijana wa umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wamesema kuwa wamemchagua Mwenyekiti wa Vijana wilaya ya Njombe ambaye atawakutanisha katika michezo kwa kuwa ni sehemu inayoweza kuwakutanisha vijana na kubadilishana mawazo na kuachana na

tabia hatarishi. 

Wakizungumza baada ya uchaguzi vijana hao wamesema kuwa kilichowafanya kumpatia ushindi Mwenyekiti Devota Kyoko ni kutokana na kujinadi kuwa atawaunganisha vijana kupitia michezo.

Mwenyekiti huyo atakaye dumu kwa muda wa miaka mitano katika kiti hicho aliyepatikana katika uchaguzi wa vijana wa chama hicho amesema kuwa vijana watatambua vipaji vyao kupitia michezo mbailimbali na kutafuta wafadhili wa vifaa vya michezo.

Aidha Kyoko amefunguka na kusema michezo inawakutanisha vijana na michezo sasa ni ajira vijana kama watatumia vizuri vipaji vyao baada ya kuvitambua watapata ajira zenye maslahi makubwa kuliko wasipo jihusisha na michezo.

"Michezo itasaidia vijana kujikinga na athari ya maambukizi ya virusi vya ukimwi,. Nimejipanga kuwatafutia vijana wafadhili mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia kwenye michezo. Nitahakikisha kila kata vijana wanapata vifaa vyite vya michezo" Bi Kyoko amesema.