Jumanne , 2nd Mar , 2021

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amemuapisha Othman Masoud Othman Sharif kuwa Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kufuatia uteuzi alioufanya hapo jana Machi 01, 2021.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Othman Masoud Othman akila kiapo mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi.

Mara baada ya kiapo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Othman Masoud Othman amesema atatumia uzoefu mkubwa alionao kumsaidia Rais wa Zanzibar kujenga na kuendeleza misingi ya maridhiano ya umoja wa kitaifa kwa maslahi mapana ya Wazanzibari.

Aidha, amesema atasaidia kujenga Serikali itakayoweza kusimamia maridhiano ya nchi ili kuendeleza amani na umoja uliopo.

Zaidi tazama video hapo chini