Jumapili , 7th Mar , 2021

Siku moja baada ya kuzagaa kwa taarifa kwenye mitandao ya kijamii, za serikali ya Kenya kuzuia uingizwaji wa mahindi kutoka Tanzania, Naibu Waziri Wizara ya Kilimo Hussein Bashe, amefika katika eneo la mpaka wa Namanga kujionea hali halisi ya undani wa jambo hilo.

Naibu Waziri Wizara ya Kilimo Hussein Bashe akiwa na viongozi wengine mpaka wa Namanga.

Kutokana na uzito wa jambo hili Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe akiwa na Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Nchini (TBS) Yusufu Ngenya, pamoja na mkuu wa kitengo cha Afya ya mimea, katika mpaka wa Namanga, ambapo kwa pamoja wameonekana kushangazwa kwa kuzuiliwa kwa malori 25 ya shehena ya Mahindi kutoka Tanzania.

Hata hivyo Bashe akawatoa wasiwasi wafanya biashara ya mazao nchini kwa kusema serikali inalifanyia kazi jambo hilo kwa uzito wa kutosha na kwa sasa wawe watulivu huku akitoa wito kwa serikali ya Kenya kutoa taarifa ya zuio hilo kwa utaratibu rasmi.

Chimbuko la sakata hili ni barua iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii na kudaiwa ni kutoka serikali ya Kenya kuzuia mahindi ya Tanzania na Uganda kuingia Tanzania.
 

Tazama Video hapo chini