Meck Sadiki, Msuya na Mujulizi wajiuzulu

Tuesday , 16th May , 2017

Rais John Magufuli ameridhia maombi ya kuacha kazi kwa viongozi watatu wa serikali kutoka katika nyanja tofauti tofauti sekta za utumishi wa Umma.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Rais Magufuli ameridhia maombi hayo ya kuacha kazi kwa viongozi hao kuanzia Mei 15, 2017.