Jumatatu , 16th Jan , 2017

Wilaya ya Pangani mkoani Tanga inakabiliwa na upungufu wa walimu takriban 27 wa masomo ya Sayansi jambo ambalo linachangia kuathiri taalum ya wanafunzi katika wilaya hiyo

Jumaa Aweso, Mbunge wa Pangani

Mbunge wa Jimbo la Pangani, Jumaa Aweso aliyeshiriki kipindi cha Weekend Breakfast siku ya Jumapili, ameiomba serikali kuchukua hatua za haraka na kuharakisha mchakato wa ajira za walimu kumaliza tatizo hilo kwa kuwa kuna baadhi ya shule wanafunzi hawana kabisa walimu.

Kuhusu walimu wa masomo ya sanaa, Aweso ambaye anaendelsha kampeni ya kuhamasisha elimu wilayani humo ijulikanayo kama 'Niaje Nisome Pangani inanitegemea', amesema walimu wa masomo hayo wapo wa kutosha na kwamba kipaumbele chao kama halmashauri kwa sasa ni ELIMU, ELIMU, ELIMU.

Mtazame hapa akielezea zaidi.........