Matibabu kwanza PF3 baadaye - Mwigulu

Thursday , 18th May , 2017

Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Mwigulu Lameck Nchemba amesema kuanzia sasa mtu yoyote atayeweza kupata majeraha yasiyokuwa na utata wapewe matibabu kwanza hospitali bila ya kuwa na kibali kutoka kwa Jeshi la Polisi (PF3) kama ilivyozoeleka.

Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba

Mwigulu ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake wa kijamii Facebook kwa kusema utaratibu huo unajicho la karibu kutoka kwenye vyombo vya usalama ili kubaini ukweli wa jeraha la muhusika.

"Tumeamua majeruhi, mahututi asiyeweza kutoroka na mtu mwenye majeraha yasiyo na utata wapewe matibabu kwanza bila PF3..Hatua za kufuata PF3 zianze mara moja wakati akiendelea kupewa matibabu, hii tunalengea kuokoa maisha yao kwanza, utaratibu huu unajicho la karibu kutoka kwenye vyombo vyetu vya usalama ili kubaini ukweli jeraha la mhusika". Ameandika Mwigulu

Mwigulu amesema hayo baada ya Jeshi la Polisi kutupiwa lawama nyingi kutoka kwa wananchi walipatwa na matatizo kushindwa kupewa huduma hospitali kwa haraka mpaka wapitie kituo cha Polisi kupatiwa cheti cha PF3 ili aende kupata huduma.

Recent Posts

Freema Mbowe

Current Affairs
Polisi msitufunge midomo - Mbowe

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Current Affairs
Tunaziba mapengo ya ajira - Majaliwa

Lulu Diva kushoto na kulia ni Linex

Entertainment
VIDEO: Linex amkataa Lulu Diva