Jumanne , 6th Dec , 2022

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amemtaka Rais wa Rwanda Paul Kagame kusitisha kile kinacholezwa kuwa uugaji mkono kwa waasi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, huku akionesha hofu juu ya ongezeko la umwagaji damu.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani. Katika mazungumzo yake na rais wa Rwanda Paul Kagame kwa njia ya simu

Blinken ameweka wazi kabisa uungwaji mkono wowote wa nje kwa makundi yenye silaha nchini Congo lazima usitishwe, likiwemo kundi la M23.

Taarifa hiyo inasema Blinken ameonesha wasiwasi mkubwa kutokana na athari za mapigano ambayo yamesababisha vifo kwa watu wa Congo, kujeruhi na wengine kuachwa bila ya makazi.

Mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu wa Marekani amezitaka nje zote mbili kujifungamanisha na makubaliano ya kuweka chini mtutu wa bunduki ya juma lililopia ya nchini Angola.