Jumamosi , 27th Mei , 2017

Idara ya jeshi nchini Marekani imesema  kwa mara ya kwanza itajaribu kudungua kombora la masafa marefu lililo na uwezo wa kufyatuliwa kutoka bara moja hadi bara lingine.

Donald Trump, Rais wa Marekani

Maafisa wa Pentagon wanasema jaribio hilo litafanyika Jumatano, wiki ijayo licha ya kuwepo na wasiwasi mjini Washington kuhusu uboreshaji wa miradi ya kinyuklia na makombora ya masafa marefu ya Korea Kaskazini.

Wasiwasi huo umeonekana kwa taifa la Marekani kuhusu mpango wa Korea ya Kusini wa kutengeza makombora mbali na mpango wake wa Kinyuklia, ambao una uwezo wa kutengeneza kombora lenye uwezo wa kufikia Marekani.