Jumapili , 27th Sep , 2020

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa amesema hafahamu lolote kuhusiana na madai ya kukamatwa kwa maafisa kampeni wa chama cha ACT-Wazalendo.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa

Akiongea na EATV/Radio Digital leo, iliyotaka kufahamu kuhusiana na madai hayo yaliyotolewa na Chama cha Siasa cha ACT-Wazalendo amesema kwamba yeye hajui suala hilo na wala hajapata taarifa zao.

Akijibu swali kwa njia ya simu lililoulizwa na mwandishi wetu wa  EATV Kamanda Mambosasa amesema kwa ufupi kwamba, “mimi sijui, wala sijapata taarifa zao”.

Maafisa wanaodaiwa kushikiliwa polisi kwa mujibu wa taarifa ya ACT-Wazalendo ni Dahlia Majid (Afisa wa Uchaguzi), Dotto Rangimoto (Afisa Habari Msaidizi) na Arodia Peter (Afisa Habari Uenezi).

Taarifa kwa umma iliyotolewa na Chama cha ACT-Wazalendo tarehe 25/ 09/2020 na Kiongozi wa chama hicho Zitto Kabwe ilielezea juu ya madai ya kushikiliwa kwa maafisa wa kampeni wa chama hicho.