Jumanne , 17th Jan , 2017

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema kuwa ukusanyaji wa mapato katika kipindi cha nusu mwaka wa fedha 2016/17 umeongezeka kwa asilimia 12.74

Richard Kayombo - Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi (TRA)

Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi Bw. Richard Kayombo imesema kuwa katika kipindi cha miezi sita ya mwaka wa fedha 2016/17 yaani kuanzia Julai hadi Desemba 2016, TRA imekusanya kodi jumla ya shilingi trlioni 7.27 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka wa fedha 2015/16.

Mlinganisho wa makusanyo kwa mwaka wa fedha 2015/16 na 2016/17 uko kama ifuatavyo:

Kayombo amesema mambo yaliyochangia ongezeko hilo ni pamoja na kuongeza ufanisi katika ukusanyaji, kuhimiza maadili mema kwa watumishi, kuboresha mifumo ya ukusanyaji, kuziba mianya ya upotevu wa mapato, pamoja na kuhimiza na kufuatilia matumizi ya mashine za kielektroniki pamoja na ukusanyaji wa kodi za majengo.

Pia amewataka wafanyabiashara kuwasilisha ritani zao za VAT kabla ya tarehe 20 kila mwezi kwa mujibu wa sheria.