Jumanne , 27th Jun , 2017

Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amesema kuwa serikali kupitia vyombo vyake inafanya jitihada za makusudi kudhibiti kuendelea kwa mauaji ya raia, askari na viongozi wa kada mbalimbali Wilayani Kibiti Mkoani Pwani.

Waziri Mkuu, Waziri Kassim Majaliwa

Mhe Majaliwa ametoa kauli hiyo jana wakati akitoa nasaha za kwenye Baraza la Idd lililofanyika kitaifa kwenye msikiti wa Riadhi,Mjini Moshi,Mkoani Kilimanjaro mara baada ya kuswali sala ya Idd.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema serikali imejidhatiti kuyakabili yanatokea wilayani Kibiti lakini ametumia fursa hiyo kuwataka raia wema kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola kwa kuwataja wale wote ambao wanahusika katika mauaji hayo.

"Tunachokifanya kwa sasa ni kuhakikisha kwamba tunawapata wahalifu halisi ili kuepuka kuingiza watu wasiohusika na kama vile hao wenye hisia kwamba mauaji yanafanywa labda na Waislamu nasema si kweli. Kazi kubwa inayofanywa sasa ni kuchuja nani hasa anayeshiriki kwenye jambo hili. Pia tunashukuru kw jinsi Watanzania wanavyojitahidi kutusaidia ni nani na nani ni wahusika" Mhe. Kassim Majaliwa.