Wakili wa mshtakiwa huyo, Joseph Makandege amedai Mahakamani hapo kuwa mteja wake asipopatiwa matibabu ya puto lililowekwa tumboni kwa muda muafaka linaweza kupasuka na kupoteza uhai wake.
Aidha, Wakili huyo ametaka mshtakiwa namba moja ambaye ni Sethi apelekwe katika hospitali ambayo ina wataalam, waliobobea kwa madai Hospitali za Magereza hazina wataalam wabobezi juu ya tatizo la mteja wake.
Kutokana na hayo kesi imeahirishwa na kusikilizwa tena hadi Septemba 29, 2017.
Mfanyabiashara Harbinder Sethi anatuhumiwa wa kesi ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha