Jumanne , 21st Feb , 2017

Kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe kufuatia kutajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda katika sakata la dawa za kulevya imeunguruma leo ambapo mahakama kuu imeweka zuio la muda kwa Mbowe kukamatwa.

Freeman Mbowe na wanasheria wake, nje ya mahakama

Akizungumza nje ya Mahakama, Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu amesema mahakama imekubali maombi ya chama hicho ya kuweka zuio kwa Jeshi la Polisi kumkamata Freeman Mbowe hadi hapo shauri hilo litakaposikilizwa, maombi ambayo yamekubaliwa.

Pia amesema mahakama imetoa nguvu kwa jeshi la polisi kumuita Mbowe kwa ajili ya mahojiano lakini si kumkamata.

Lissu amesema maamuzi mengine yaliyotolewa na mahakama ni kumtaka mleta maombi ambaye ni Mbowe, kufanyia marekebisho maombi yao kwenye shauri la msingi kwa kumuingiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Maombi hayo yanayohusu zuio la Mbowe kukamatwa yatasikilizwa tena kesho kutwa Februari 23 katika mahakama ya wazi, lakini kesi yenyewe itasikilizwa terehe 8, mwezi Machi baada ya kuwa wamefanyia marekebisho maombi yao.

Huyu hapa Tundu Lissu akifafanua