Jumatatu , 22nd Mei , 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Adolf Hyasinth Mohondela Ndunguru kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, TRA .

Rais Magufuli akiwa kazini

Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu imesema, uteuzi wa Bw. Ndunguru umeanza leo .

Kabla ya uteuzi huo Bw. Ndunguru alikuwa Kamishna wa Sera, katika Wizara ya Fedha na Mipango.

Bw. Adolf Ndunguru anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Charles Edward Kichere ambaye hivi karibuni aliteuliwa kuwa Kamishna Mkuu wa TRA.