Jumatatu , 21st Sep , 2020

Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Magufuli, akiwa katika mwendelezo wa kampeni zake za urais leo Septemba, 21, katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora, amegusia suala la vitambulisho vya machinga ambavyo hupatikana kuwa ni utaratibu unaowalinda wajasiriamali wadogo

Mgombea Urais kupitia CCM Dkt John Magufuli

''Vitambulisho havilazimishwi ni lazima itolewe elimu kwa wanaoshiriki kwenye vitambulisho iliwakafanye bishara mahali popote, tunataoa vitambulisho ili wanananchi hawa wenye biashara ndogondogo wasisumbuliwe''. Dkt John Magufuli, Mgombea urais kwa tiketi ya CCM.

Aidha amewataka wasaidizi wake wakiwamo wakuu wa wilaya kuendelea kuzingatia maelekezo yake ni wafanyabiashara wa aina gani wanaohitajika kuwa na vitambulisho vya machinga. 

Vitambulisho hivyo humwezesha mjasiriamali kufanya baishara bila kutozwa kodi na halmashauri kwa kipindi cha mwaka mzima jambo ambalo hutajwa kuwa linalenga kuwainua wafanyabiashara wa mitaji midogo.

''Tulianzisha vitambulisho hivi kwaajili ya kuwalinda wafanyabiashara wadogo wadogo baada ya kuona wanasumbuliwa na halmashauri, ukiwa na kitambulisho chako utafanya biashara mahali popote Tanzania, vitambulisho haviwezi vikatafutwa kwa bunduki, vitambulisho mtu anakata mwenyewe ni Sh 20000'' Dkt John Magufuli, Mgombea urais kwa tiketi ya CCM.