Alhamisi , 21st Jan , 2021

Rais Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa familia, ndugu na Spika wa Bunge, Job Ndugai, kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Manyara kupitia CCM Martha Umbula, na kusema kuwa marehemu alikuwa mpole, mchapakazi na mpenda maendeleo.

Kushoto ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli na kulia ni Martha Umbula wakati wa uhai wake

Taarifa hiyo imetolewa leo Januari 21, 2021, na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa, na kwamba Rais Magufuli, anakumbuka jitihada zake za uongozi akiwa mkuu wa wilaya na mbunge na kuwaomba wanafamilia wawe na moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.

Kifo cha Martha Umbula, kimetokea usiku wa kuamkia leo kilichotokea nchini India, katika Hospitali ya HCG Mumbai, alipokuwa anatibiwa na Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia inaratibu mipango ya mazishi