Alhamisi , 12th Jan , 2017

Siku moja baada ya Mbunge wa Kilombero Mhe. Peter Ambrose Lijualikali kuhukumiwa na Mahakama kwenda jela miezi 6, Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimeandaa timu ya wanasheria kwa ajili ya kuanza taratibu za kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo

Tundu Lissu

Akizungumza na vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam, Mwanasheria Mkuu wa chama hicho na Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Mhe. Tundu Lissu amesema timu ya wanasheria wa chama hicho wameanza taratibu za kukata rufaa, kwa kuandaa notisi ya rufaa na maombi ya dhamana ya dharura wakati uamuzi juu ya rufaa yake ukisubiriwa ili Mhe. Lijualikali  aweze kupata dhamana huku wakiendelea na kesi hiyo.

Aidha, Mhe. Lissu amesema, hukumu hiyo kwa Mhe. Peter Lijualikali haina athari zozote kwa hadhi yake kama mbunge wa jimbo la Kilombero kwani Katiba imeeleza wazi juu ya makosa yanayoondoa sifa za kuwa mbunge na kwamba adhabu ya kifungo alichopewa haijazidi miezi 6 na kosa alilohukumiwa siyo kosa la kugushi, ubadhirifu ama makosa mengine yanayoambatana na utovu wa uaminifu.

Peter Lijualikali