Ijumaa , 30th Oct , 2015

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kimelilalamikia jeshi la polisi kwa kuwakamata wafanyakazi wake zaidi ya 40 kwa sababu zisizofahamika na kulitaka jeshi polisi kutoa taarifa ya sababu za kukamatwa kwao.

Mwanasheria kutoka kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC ndugu HAROLD SUNGUSIA akizungumza na wanahabari

Akizungumza na waandishi mwanasheria wa kituo hicho Bw. Harlod Sungusia amesema jeshi la polisi lilivamia kituo chao cha kukusanya taarifa za uchaguzi ka kukusanya komputa na kisha kuondoka na wafanyakazi hao bila kupewa maeleoz yoyote.

Sungusia amesema kituo cha kina kibali kutoka tume ya taifa ya uchaguzi NEC inayowaruhusu kufuatilia mwenendo wa uchaguzi kwa kuchukua matoke ambayo ni rasmi kutoka tume hiyo na baadae kutoa taarifa juu ya mwenendo wa Uchaguzi ulivyokwenda.

Bw. Sungusia ambaye alikuwa akiongea wakati zoezi hilo la upekuzi likiendelea ameshangaa kwa hatua hiyo ya polisi kwani wao wana kibali kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kufanya shughuli za uangalizi na kuandika ripoti.

Sungusia amesema wamejipanga kwenda kudai haki yao kisheria ikiwa ni pamoja na kuwasimamia vijana hao ikiwa ni pamoja na kupata maelezo ya kutosha juu ya kukamatwa vijana hao ambao anadaia kuwa walikuwa wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria.