Jumapili , 20th Aug , 2017

Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Jonathan Lema amemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi Simon Sirro kulifundisha jeshi lake kufanya kazi kwa weledi na kwamba siyo kila amri wanayopewa na viongozi wa mikoa na wilaya inaweza kuwa afya kwa taifa la Tanzania.

Mhe. Lema amesema hayo leo baada ya kuzungumzia suala la kamata kamata inayofanywa kwa amri ya wakuu wa wilaya na mikoa na kusema kwa jinsi jeshi la polisi linavyotumika siyo kila amri itakyotolewa itakuwa na maana ndani ya nchi kwani zigine zitalipeleka pabaya taifa la Tanzania.

"Hizi amri ambazo zinatolewa na kutekelezwa sizo nzuri. Mfano DC siku akisema  Mbunge wa Arusha mjini apigwe risasi basi amri hiyo itatekelezwa nitapigwa. Kwa staili hii najua wapo watu ambao watakuja nyuma yetu au wengine ambao tupo nao sasa hivi watashindwa kuvumiliwa haya mateso na udhalilishwaji, ambao  haipiti wiki mbinge wa upinzani anakuwa amekamatwa. Nakemea sana jambo hili," Lema alifunguka.

Pamoja na hayo Mhe. Lema amempongeza Rais Mteule wa Kenya, Mh. Uhuru Kenyatta kwa kuonyesha demokrasia ya kweli ya kuruhusu maandamano ya kuupinga ushindi wake huku akitoa na jeshi la kuwalinda raia katika maandamano hayo.