Jumanne , 15th Sep , 2015

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewateua Makamishna wawili wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC pamoja na wakuu wa mikoa wawili ambao wanaziba nafasi zilizoachwa na wakuu wa mikoa walioingia kwenye kinyang'anyiri cha kugombea ubunge.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete (pichani) amewateua Makamishna wawili wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue imesema kuwa uteuzi huo ulianza jana kwa makamishna hao wa NEC ambao ni Jaji Mstaafu wa Mahakama kuu ya Tanzanoa Mary Longway na wakili wa kujitegemea Asina Omary.

Aidha Taarifa nyingine iliyotolea na Balozi Sefue ni Kumteua Amos Makalla kuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro na Jordan Rugimbana kuwa mkuu wa mkoa wa Lindi huku Mwantumu Mahiza akitoka Lindi na kuhamishiwa Tanga na Said Magalula akitokea Tanga na kupelekwa Rukwa kuchukua nafasi ya mhandisi Stela Manyanya.

Makalla ambaye ni mbunge aliyemaliza muda wake katika jimbo la Mvomero anachukua nafasi ya iliyoachwa wazi na Leonidas Gama ambaye anawania ubunge mkoani Ruvuma.