Alhamisi , 19th Oct , 2017

Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Kangi Lugola amesema kashfa ya rushwa iliyokuwa inamkabili kipindi cha serikali ya awamu ya 4, ilikuwa ni zengwe alitengenezewa baada ya kutaka kufichua vitendo vya rushwa.

Kangi Lugola ameyasema hayo leo alipokuwa kwenye kipindi cha East Africa Breakfast kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kwamba wakati yupo kwenye mchakato wa kufichua vitendo viovu vilivyokuwa vikifanywa na serikali, ndipo akatengenezewa zengwe na mtu ili aache kufanya hivyo.

Kangi Lugola ameendelea kusema kwamba inafahamika wakati wa awamu ya nne alikuwa kinara kwenye kuikosoa serikali ya CCM ambayo pia ndio chama chake, na alikuwa wa kwanza kutia saini ya kutokuwa na imani na waziri mkuu wa awamu ile.

Mtazame hapa chini