Jumapili , 19th Feb , 2017

Jumuiya na Taasisi za Kiislam imepongeza vita dhidi ya dawa za kulevya na kupendekeza kuwa kamata kamata ya wahusika wa dawa za kulevya inayoendelea hivi sasa ihusishe pia wapiga debe wanaoonekana katika vituo vya daladala wakiwa wameathirika

Kaimu Msemaji wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam, Sheikh Rajab Katimba, ametoa wito huo jijini Dar es Salaam leo katika mkutano wake na wanahabari na kwamba vita dhidi ya dawa za kulevya haitakuwa na maana kwa wachache kukamatwa na wengine kuachwa.

Sheikh Katimba amesema jamii hususani Jumuiya ya Taasisi za Kiislam inategemea kuona wahusika wote wa dawa za kulevya wakikamatwa na kufikishwa mahakamani kuliko ilivyo hivi sasa ambapo taasisi hiyo inadai kuwa baadhi ya watu inaodhani kuwa ni watumiaji wa dawa za kulevya wakiwa wameachwa huku wengine wakikamatwa hali inayoleta hofu juu ya malengo hasa ya vita hiyo