Jumatatu , 25th Sep , 2017

Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata) wamemuomba Rais Magufuli, kurejesha kwa Watanzania mchakato wa uandikwaji wa katiba mpya kwa madai hiyo ndiyo njia pekee ya kuonyesha dira ya nchi na kuendeleza mazuri yanayofanywa na uongozi wa awamu ya tano.

Profesa Gaudensi Mpangala ambaye ni mhadhiri wa chuo kikuu cha katoliki Ruaha ametoa ushauri huo katika mkutano wa mafunzo ya wanachama wa Jukwaa la Katiba mjini Dodoma juu ya hatma ya mchakato wa katiba mpya nchini ukiwa na lengo la kupatikana kwa  Katiba itakayosaidia kuonyesha dira ya nchi na kukuza uchumi wa wananchi mmoja mmoja.

Naye Mkurugenzi wa Jukwaa la Katiba, Hebron Mwakagenda amesema kutokana na mambo mazuri yanayofanywa na serikali ya awamu ya tano kwa sasa, yanapaswa kuwepo katika Katiba mpya ili yaendelezwe.