Alhamisi , 14th Sep , 2017

Wabunge wa chama cha Jubilee Kenya wamepeleka maombi kwenye Tume ya Utumishi wa Mahakama (JSC) kumuondoa madarakani Jaji Mkuu wa wa Mahakama ya Juu , David Maraga ikiwa ni wiki chache baada ya jaji huyo kutengua matokeo ya urais .

 Mbunge wa Nyeri Mjini , Ngunjiri Wambugu amefungua mashtaka hayo leo katika Tume ya Majaji akitaka Jaji Maraga ang’olewe kwa kile alichokieleza kuwa utendaji wake ni mbaya.

Wambugu  amewasilisha mashtaka yenye kurasa 14 na  ameomba Tume ya Majaji kwa kushirikiana majaji na mahakimu kuanzisha uchunguzi dhidi ya Jaji Maraga ili kubaini mwenendo wake tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo.

Chama cha Jubilee wanataka jaji huyo achunguzwe kutokana na kuhusishwa na mashirika ya kiraia yanayompinga Rais Kenyatta  Nairobi, Kenya.

Kwa mujibu wa Chombo cha habari Kenya kimeandika kuwa Mbunge huyo amedai jaji huyo alimzuia Jaji Mohamed Ibrahim kushiriki katika kesi iliyofunguliwa na mgombea wa Nasa, Raila Odinga aliyekuwa akipinga matokeo ya urais. Jaji Ibrahim alishindwa siku ya pili kusikiliza kesi hiyo kutokana na kuugua.

Septemba 1 mwaka huu Jaji David Maraga alibatilisha matokeo ya Urais yaliyompa ushindi Mgombea wa Jubilee Uhuru Kenyata kupitia kesi iliyofunguliwa na Muungano wa vyama vya upinzani Nasa kwa kusema kuwa uchaguzi ulikuwa na dosari