Jumanne , 8th Sep , 2020

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Jummanne Shauri amesema kukamilika kwa miradi ya kimkakati katika Manispaa hiyo ikiwemo Machinjio mpya ya kisasa inayojengwa Vingunguti kunatarajiwa kutoa ajira za kudumu zaidi ya 200 na watu wengine zaidi ya 3,000 kushiriki katika nyanja mbalimbali.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Jummanne Shauri akiwa katika moja ya matukio muhimu picha na maktaba.

Hii leo Eatv imefika ofisini kwake na kufanya mazungumzo juu ya namna miradi ya kimkakati itakavyo wanufaisha makundi mbalimbali mkurugenzi huo emeelezea jinsi wanavyotarajia kuanzisha viwanda vidogo vidogo vilivyolenga kunufaisha makundi mbalimbali.

Wakati huo huo Bw Shauri amesema kwa muhula huu wa kwanza unaokwenda kuishia Manispaa inatarajia kutoa shilingi bilioni moja kwa ajili ya mikopo rahisi kwa makundi ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo hadi kufiki sasa vijana wengi wamenufaika kwa mikopo ya bodaboda na bajaji huku vikundi vingine vilipewa basi pamoja na gari ya kuchakata taka taka.