Ijumaa , 10th Nov , 2017

Majaji katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, wametoa idhini kwa Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama hiyo, Fatou Bensouda, kuanza uchunguzi wa tuhuma za uhalifu wa kivita nchini Burundi.

Majaji hao walitoa idhini hiyo Oktoba 25 mwaka huu, ikiwa ni siku mbili kabla ya Burundi kutangaza kujitoa katika Mahakama hiyo Oktoba 27.

Katika uamuzi wao Majaji wamebaini kwamba, kuna sababuz a msingi za kufanyika kwa uchunguzi huo kuhusiana na uhalifu dhidi ya binadamu.

Takriban watu 1,200 wameuwawa katika machafuko nchini Burundi tangu mwaka 2015, ambao taarifa za idhini hiyo zilichelewa kutolewa ili kutoa muda wa kuweka mazingira ya kuwalinda waathirika na mashahidi.