Jumamosi , 23rd Sep , 2017

Baada ya Bunge kusema wametuma fedha za matibabu ya Mbunge Tundu  Lissu tangu Septemba 20, Hospitali ya Nairobi imekiri kupokea fedha kutoka Tanzania zikiwa hazina maelezo na wanafanya kuzifuatilia.

Afisa wa Kitengo cha Habari na Itikadi wa Chadema, Hemed Ali amesema Hospitali na Nairobi nchini Kenya imethibitisha kupokea fedha kutoka Tanzania lakini zikiwa hazina maelezo.

 Jana ofisi ya Bunge ilitoa taarifa kuelezea mchakato wa utumaji wa fedha hizo kiasi cha Sh 43 milioni zilizochangwa na Wabungea wa Tanzania ikisema kuwa pesa hizo zilitumwa tangu Septemba 20.

Ofisi ya Bunge ililazimika kufafanua kuhusu fedha hizo ikiwa ni muda mfupi tu baada ya  na  taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe alipokuwa akizungumza na wanahabari na kusema kuwa michango mingio alikwishapokea isipokuwa mchango huo wa wabunge uliokuwa na thamani ya milioni 43

Ali ambaye yupo Jijini Nairobi  Nairobi amesema amethibitishiwa na Hospitali ya Nairobi kuwa wamepokea fedha hizo kutoka Tanzania ingawa kulikuwa hakuna maelezo zaidi.

“Wamenieleza kuna fedha zimeingizwa kutoka Tanzania ila hazina maelezo ndiyo wanafuatilia benki,” amesema Afisa habari Ali