Jumapili , 24th Jan , 2021

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Tanzania ina usalama mzuri wa chakula na hakuna njaa nchini ukiacha mapungufu tu.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Ameyasema hayo wakati akizindua mwongozo wa uwekezaji mkoa wa Iringa ambapo amesisitiza kwamba Serikali itaendelea kudumisha amani na utulivu ambao ni muhimu kwa wawekezaji na wananchi.

''Serikali ya awamu ya tano inajivunia sana wawekezaji nyie ndio chachu ya maendeleo, kuongeza ajira na kuimarisha uchumi. Kwasasa Tanzania tunajivunia kuwa na usalama mzuri wa chakula, hatuna njaa tuna mapungufu tu na hiyo ni nyie wawekezaji'' ameeleza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Waziri Mkuu pia amewataka watendaji wote wa Serikali katika ngazi mbalimbali kushiriki kutangaza fursa za uwekezaji na pia kutatua changamoto mbalimbali zilizopo katika sekta wanazozisimamia ili kurahisisha mazingira ya biashara na uwekezaji katika maeneo mbalimbali nchini.

Tazama Video hapa chini