Jumatano , 20th Oct , 2021

Mkurugenzi wa TEHAMA Wizara ya Habari, Teknolojia na Mwasiliano ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kongamano la Tano la Mkutano Mkuu wa TEHAMA 2021, Mulembwa Munaku, amesema jitihada mbalimbali zinaendelea kuchukuliwa ili kufikia taifa la kidijitali.

Mkurugenzi wa TEHAMA Wizara ya Habari, Teknolojia na Mwasiliano

Munaku ameyasema hayo leo kwenye Ukumbi wa Simba ndani Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha wakati akieleza muelekeo wa kidijitali kama taifa na jitihada mbalimbali zinazoendelea katika kufikia uchumi wa kidijitali.

''Kama ambavyo tunafahamu 75% ya wananchi ni vijana, ni wazi tunahitaji kuwekeza zaidi kwenye TEHAMA ili kuwawezesha kujikwamua ikiwemo kupata ajira na kujiajiri wenyewe kupitia teknolojia katika ulimwengu huu wa kidijitali, kwasababu ni asilimia 25 ndio wanapata ajira rasmi,'' amesema Mulembwa Munaku.

Aidha ameongeza kuwa, ''Mahitaji bado ni makubwa kwenye uwekezaji wa kufikisha 'internet' kwenye maeneo ya vijijini, hata hivyo tunayashukuru makampuni mbalimbali ya mitandao ya simu kwa kuendelea kufikisha huduma katika maeneo hayo,''.