Alhamisi , 25th Feb , 2021

Mahakama  ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemuachia huru Mbunge wa Viti Maalum wa CHADEMA, Halima Mdee, baada ya upande wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yake kuwa alitoa maneno machafu dhidi ya Rais Magufuli.

Mbunge wa Viti Maalum, Halima Mdee

Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thamos Simba ambapo amesema Mashahidi watatu (Askari) wa upande wa mashtaka, wameshindwa kuthibitisha kuwa Mdee alitoa maneno ya uchochezi, kwa hiyo mshtakiwa hana hatia na Mahakama imemuachia huru.

"Upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha mashtaka dhidi ya mshtakiwa, kwa hiyo Mdee hana hatia, Mahakama ina muachia huru na haki ya kukata rufaa ipo wazi” Hakimu Simba

Mdee anadaiwa kuwa July 03,2017 katika makao makuu ya ofisi ya CHADEMA yaliyopo mtaa wa Ufipa wilayani Kinondoni, alitenda kosa la kutoa lugha chafu.