Godbless Lema atabiri tena

Monday , 19th Jun , 2017

Mbunge Godbless Lema amefunguka na kutoa utabiri mwingine mpya kuwa katika nchii hii baada ya miaka 15 au 20 kila nyumba itakuwa na watu waliomaliza shahada ya kwanza na 'masters' lakini hazitakuwa na tija katika maisha yao na nchi kwa ujumla.

Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA) Mhe. Godbless Lema.

Godbless Lema amesema hayo alipokuwa katika mahafali ya Umoja wa wanafunzi wa elimu ya juu wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHASO) ambapo amewataka wanafunzi hao kuwa na maadili na maono katika maisha yao huku akisema hata katika vita ambayo nchi inapigana sasa, watu wanaoturudisha nyuma ni wasomi ambao wameshindwa kutambua wajibu wao.

"Ambalo mimi naliona ni vijana wenye vyeti lakini hawana 'moral authority' nchii hii baada ya miaka 15 au 20 kutoka sasa utakuta kila familia ina degree, kila familia ina masters lakini zisizona tija. Wasomi wasio na moral authority ni hatari kuliko wajinga wenye moral authority na gata ukiangalia kwenye haya mapambano wanaofanya kazi yetu inakuwa ngumu ni wasomi ambao wameshindwa kujua wajibu wao" alisema Godbless Lema 

Mbali na hilo Lema amesema wasomi wengi wa sasa ambao ni vijana wamekuwa ni watu wasiojali mambo ya msingi, wamekuwa wakijali sana mambo yasiyokuwa na tija katika nchi au taifa na kuikacha siasa ambayo ndiyo msingi wa kila kitu. 

"Vijana wa sasa hamjali mnajua mambo ya mipira, yaani vijana wasomi wa nchi hii wanajua zaidi mipira sijui 'Premier League' mimi siyajui vizuri hayo mambo, yaani 'commitment' yenu kwenye mambo ambayo hayawezi kuleta tija kwenye nchi imekuwa kubwa kuliko 'commitment' yenu kwenye mambo ya siasa" alisisitiza  Lema 

Recent Posts

Simon Msuva na Haruna Niyonzima

Sport
Msuva amlilia Niyonzima

Makamu wa Rais Samia Suluhu

Current Affairs
Serikali yetu haitarudi nyuma - Samia

Rais Magufuli.

Current Affairs
Rais Magufuli awachimba biti wanafunzi

Katibu Mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa

Sport
Mkwasa kuwashika koo waliochoma jezi

Msanii Dogo Janja Kushoto, na Kulia ni Mfanyabiashara Muna Love

Entertainment
Dogo Janja aruka kwa Muna Love