Jumatano , 13th Sep , 2017

Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala na Omari Kumbilamoto (CUF) amefunguka na kusema kuwa anakisikitikia chama chake kwani kinakatisha tamaa kutokana na mgogoro unaoendelea na kuwaomba waanahabari kutumia weledi na ushawishi wao kumaliza mgogoro huo.

Omari Kumbilamoto

Akizungumza leo asubuhi kwenye kipindi cha East Africa Breakfast, kinachorushwa na East Africa radio,  Mh.  Kumbilamoto ambaye pia ni Diwani wa kata ya Vingunguti (CUF) amesema kwamba chama cha CUF kilikuwa ni kimbilio la wananchi wanyonge lakini kwa sasa kimekuwa ni cha kilio kuanzia viongozi mpaka wanachama wenye mapenzi ya dhati.

"Cuf inatia huzuni.....Inahitaji maombi ili migogoro iishe....Nawaonea sana huruma viongozi hasa madiwani ambao huu mgogoro unawaumizwa kwa sababu 2020 ni siku chache zijazo na kama hawajafanya kitu hawataweza kuwaambia kwamba hajafanya maendeleo kwa sababu ya mgogoro wa chama na wakamuelewa. Viongozi wa CUF, Wabunge na wengineo wafanye kazi na huu mgogoro usiwaumize wakashindwa kuwatumikia wananchi.

Kumbilamoto ameongeza "Waandishi wa habari na nyie pia mna uwezo wa kufanya haya mambo yaishe kwa kutumia kalamu zenu pamoja na hekima zenu kwa sababu hata vitabu vya dini vimewataja".

Mbali na hayo kiongozi huyo amesema hana mpango wa kuendele kung'ang'ania madarakani endapo pale umri wake wa kuwa kwenye siasa utakuwa umekwenda na kwamba atahitaji mapumziko kwani kiongozi mwenye nia ya kutumikia wananchi huwa haoni utamu wa uongozi.

Msikilize zaid hapa

Kumbilamoto akiwa kwenye kipindi cha East Africa Breakfast