Jumanne , 17th Jan , 2017

Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA), Freeman Mbowe, amesema wamefanikiwa kufanya ziara na mikutano ya ndani na kukutana na kata zote za Kanda ya Ziwa kwa ajili ya maandalizi ya mkutano mkuu wa chama hicho.

Freeman Mbowe

 

Akizungumza na wanahabari jijini Mwanza hii leo, Mh. Mbowe amesema, kesho kutakuwa na mkutano mkuu wa Kanda ya Ziwa kwa Mikoa ya Kagera, Geita na Mwanza ambao utahudhuriwa na viongozi wote pamoja na wabunge mbalimbali wa chama hicho.

Mh. Mbowe amesema mikutano ya ndani imesaidia kukiimarisha chama na kuwapa nafasi ya kukutana na viongozi wote wa mitaa na kata pamoja na madiwani kwa ajili ya kufanya tathmini kuhusu ya uchaguzi mkuu.