Alhamisi , 23rd Mar , 2017

Aliyekuwa Waziri wa Habari, Sanaa utamaduni na michezo Nape Nnauye ambaye leo ametenguliwa na Rais Magufuli amefunguka na kusema leo mchana atakutana na waandishi wa habari kutoa ufafanuzi wa jambo hilo. 

Nape Nnauye ambaye ni Mbunge wa jimbo la Mchinga amesema hayo kupitia mtandao wake wa twitter 

"Ndugu zangu naomba tutulie! leo mchana nitakutana na Wanahabari na tutalizungumza hili. Nitawaambia saa na mahali, kwasasa naomba tutulie" Nape Nnauye 

Rais Magufuli leo asubuhi amefanya mabadiliko madogo ya baraza lake la Mawaziri kwa kumteua Dr. Harrison Mwakyembe kuwa Waziri wa Habari, Sanaa utamaduni na michezo. ambaye ilikuwa chini ya Nape Nnauye pia amemteua Prof. Palamagamba Aidan John Mwaluko Kabudi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.

 

ALIYOZUNGUMZA NAPE NNAUYE NA WANAHABARI LEO

"Lengo langu kwanza ilikuwa ni kumshukuru Rais kwa uamuzi alioufanya pamoja na kwa kuniamini kwa mwaka mmoja"- Nape Nnauye

"Mimi Nape sina kinyongo na uamuzi wa Rais wangu, sina sababu ya kuupinga uamuzi wake" - Nape Nnauye

"Nawaomba muungeni mkono Rais Magufuli, huyo ndiye Rais tuliyenaye, ndiye Rais tuliyepewa na mwenyezi Mungu" - Nape Nnauye

"Niko hapa kuwashukuru wanahabari kwa ushirikiano mlionipa kwa mwaka mmoja, nimewapenda sana sana sana" - Nape Nnauye

"Nilisema kuna gharama ya kulipa katika kusimamia haki za watu, na mimi niko tayari kulipa gharama hiyo" - Nape Nnauye

"Tusihangaike na Nape, tuhangaike na Tanzania, 
Nape ni mdogo sana kuliko nchi" - Nape Nnauye

"Tusije tukamgeuza Nape akawa mbadala au mkubwa kuliko Tanzania, Tanzania ni kubwa kuliko Nape" - Nape Nnauye

"Vijana wenzangu hamna cha kuogopa, simamieni mnachokiamini". - Nape Nnauye

Mtazame hapa.........