Jumanne , 23rd Mei , 2017

Msanii wa hip hop, Kala Jeremiah amemuomba Waziri Mwakyembe kutengua kauli yake ya kuwataka wasanii waache kuimba nyimbo zinazohusu siasa, kwa madai kuwa ni kuwatenga mbali na jamii inayotegemea wasanii kuwasemea mahitaji yao.

Akizungumza kwenye 'story' tatu ndani ya Planet Bongo, Kala amesema kuwa kauli ya  Mh. Mwakyembe haiko sawa kwani inatengeneza 'gap' kubwa kati ya jamii na wasanii na kuongeza kwamba siasa zinazoimbwa na wasanii ndizo ambazo zinasaidia jamii na wakati mwingine zinasaidia serikali kutopoteza pesa.

Aidha Kala amendelea kufunguka kwamba yeye kama msanii anayeimba harakati kwa ajili ya kusaidia jamii yake kauli ya Waziri ni kama inamlazimisha kuimba nyimbo za mapenzi kitu ambacho kwake hakitampa tatizo lakini hasara itakuwa kwa jamii inayohitaji kusemewa.

 Pamoja na hayo Kala amefunguka na kusema wimbo wake alioimba kuwasemea watoto yatima 'Wanandoto' umempatia sifa kubwa kutoka kwenye mashirika mbalimbali yanayojihusisha na kusaidia watu wenye matatizo na kumpongeza kwa kuweza kufikisha ujumbe mzito pasipo kutumia gharama kubwa sana.

Msikilize hapa chini Kala akifunguka kwa undani zaidi.