Jumatatu , 21st Aug , 2017

Meya wa Manispaa ya Ubungo Mh. Boniface Jacob, amelezea tukio la bomoa bomoa linaloendelea katika maeneo ya Kimara na kuathiri wakazi wake kuwa ni la uonevu na lenye kubebwa kisiasa.

Meya wa Manispaa ya Ubungo Boniface Jacob

Akizungumza na East Africa Radio, Boniface Jacob amesema kitendo hicho kimekuwa cha uonevu kwa sababu kesi bado iko mahamani, lakini serikali imetoa amri nyumba hizo zibomolewe, bila kusubiria hatma ya kesi.

Boniface Jacob pia ameelezea tukio hilo limebebwa na sura ya kisiasa na kusema kuwa kitendo cha wakazi wa maeneo hayo kuwa upande wa vyama vya upinzani ndiyo umewagharimu, na kufanyiwa vitendo vya uonevu wa hali ya juu.

Eneo la Kimara kumefanyika zoezi la kubomoa nyumba na ambalo limeonekana kuathiri kiasi kikubwa cha wakazi wa maeneo hayo, na kuibua malalamiko mengi kwa watanzania ambao hata siyo wakazi wa maeneo haya.

East Africa Radio ilifanya jitihada za kumtafuta Afisa Mtendaji Mkuu TANROADS, Mhandisi Patrick Mfugale ili iweze kuweka bayana suala hilo, na kusema kuwa kitu ambacho yeye anafahamu kesi ya mahakamani iliisha tangu mwaka 1993 na serikali ilishinda, hivyo walikuwa na amri napo, lakini kabla ya kuanza zoezi la ubomoaji walishatoa 'notice' kwa wakazi hao ili waweze kutoka maeneo hayo.

Sikiliza maongezi ya watu wote wawili wakelezea suala hilo

Alichokizngumza Meya wa Manispaa ya Ubungo kuhusu bomoa bomoa Kimara
Alichosema Afisa Mtendaji Mkuu TANROADS, Mhandisi Patrick Mfugale
Afisa Mtendaji Mkuu TANROADS, Mhandisi Patrick Mfugale