Jumatano , 23rd Aug , 2017

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mh. Anna Mgwira amekiri kupokea malalamiko ya chama cha walimu mkoa wa Kilimanjaro (CWT) kumtaka ahakikishe Mkuu wa wilaya ya Hai, Mh.Gelasius Byakanwa anaomba radhi kwa walimu kwa kitendo cha kumdhalilisha mwalimu mwenzao

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, mama Anna Mghwira

Akizungumza na mwandishi wa East Africa Radio, Mama Anna Mghwira amesema taarifa hizo amezipokea na ofisi yake itafanyia kazi suala hilo, kadri walalamikaji walivyohitaji kwa kuwa wana haki ya kulalamikia suala hilo.

“Imefika na wameleta na sisi tumewaambia tutayafanyia kazi yale yanayotuhusu, ilikuwa ni lazima waje kuniona, kuna mapendekezo mengine ambayo yapo ndani ya mamlaka yao, kwa mfano wakisema wenyewe baada ya siku 30 wanataka kufungua kesi, nani atawazuia!? Hata ikiwa ni siku moja, ni haki yao, ni jukumu letu tunajua ilivyotkea, tunafuata taratibu za kawaida za kazi”, alisema Mama Anna Mghwira.

Mkuu wa wilaya ya Hai, Mh.Gelasius Byakanwa alifika shule moja iliyopo ukanda wa chini mwa wilaya ya Hai, na kumtaka mwalimu mmoja apige push up kwa kushindwa kujibu swali alilo uliza, ndipo akamuitia polisi na kumpeleka rumande bila kosa kisheria.

Msikilize hapa chini Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mama Anna Mghwira.