Aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mama Anna Elisha Mghwira
Imeelezwa kuwa Mama Mghwira amefariki dunia leo Julai 22, 2021, majira ya mchana, ambapo taarifa zinadai kwamba wiki moja iliyopita alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Nkoaranga kwa tatizo la kupumua ambapo baadaye hali yake kuwa mbaya alihamishiwa hospitali ya Mount Meru.