Alhamisi , 19th Oct , 2017

Mhubiri wa kanisa la The Remnant ambaye alitabiri kuwa Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe angefariki siku ya Jumanne,  amejitetea mahakamani kwamba utabiri wake haukutimia, akisema kuwa Mungu amebadilisha fikra zake.

Mhubiri huyo raia wa Zimbabwe Philip Mugadza amedaiwa kuishawishi mahakama ya juu nchini humo kutupa kesi dhidi yake kwa kutabiri kuwa Rais Robert Mugabe, 93, angefariki tarehe 17 mwezi Oktoba mwaka 2017.

"Sababu iliyosababisha Mungu kuhairisha hili, hakuniambia, kwa hivyo sijui ni kwa nini Mungu aliamua kuchukua mkondo huo. Ninajua watu wengi walikuwa wakitarajia kutimia kwa unabii kwa sababu ya kile kinachoendelea nchini mwetu."

Wakili wa Muhubiri huyo Gift Mtisi ameiambia BBC kuwa  mteja wake anakubali kuwa alisema maneno hayo na hakudanganya na kwamba huo ni ujumbe kutoka kwa Mungu, hivyo "Polisi watahitaji kuthibitisha kuwa Mungu hakusema hilo."

Aidha Mawakili wa Muhubiri huyo wameitaka mahaka ya katiba kutupilia mbali mashtaka hayo kwa misingi kuwa yanakiuka haki yake ya uhuru wa kusema.

Mwendesha mashtaka anasema kuwa muhubiri huyo alitukana dini ya kikiristo na tamaduni za Afrika kwa kutabiri kifo cha Mugabe na kwamba kutabiri kifo cha kiongozi ni mwiko, kulingana na imani za kitamaduni na Kesi hiyo imeahirishwa.