Jumamosi , 21st Oct , 2017

Diwani wa Mbuguni, Bw. Ahimidiwe Ali Rico amesema kwamba watu wasihamishe mjadala wa kuhusu mamlaka ya kurekodi madiwani waliohama Chama cha demokrasia na Maendeleo, CHADEMA na badadala yake mjadala ni kuhusu kupambana na rushwa.

Bw. Ahimidiwe amesema kwamba hana unafki wala nidhamu ya uoga ndiyo maana aliamua kufanya kazi hiyo ili kulikomboa taifa kutoka kwenye harufu ya rushwa na kuwataka wanaozusha maneno watulie kabla hajawaaibisha zaidi.

Diwani huyo ameweka wazi kwamba mkakati huo wa kurekodi na kuwachunguza viongozi wanapokea na kutoa rushwa ulianza muda mrefu na kwamba yupo makini katika hilo na wala siyo filamu kama jinsi ambavyo wanasiasa hao walivyoanza kuzusha.

"Mchezo uliokuwa unafanywa Arumeru nilianza kuufanyia kazi muda mrefu baada ya kuona madiwani wanaondoka kama njugu. Ushahisdi wa kifaa kilichotumika kipo tyayari Takukuru na sijataka kuingilia ushahidi wao hivyo ni jukumu lao kuonyesha kwa watanzania namna haki inavyotendeka" Ahimidiwe