Aliyekuwa Mkurugenzi ATCL ahukumiwa kwenda jela

Wednesday , 13th Sep , 2017

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) David Mataka na aliyekuwa Kaimu Ofisa Mkuu Kitengo cha Fedha ambaye ni Askofu wa Kanisa la Pentecoste Motomoto, Elisaph Mathew.

Wawili hao wamehukumiwa kifungo cha miaka 6 jela ama kulipa faini ya Sh.milioni 35 kwa kila mmoja kutokana na mashtka yao sita waliyokuwa yanawakabiri pia Mahakama imewataka washtakiwa hao kulipa hasara waliyoisababishia ATCL kwa kununua magari chakavu 26, yalikuwa na thamani ya zaidi ya dola milioni 143 ndani ya mwezi mmoja.

Kwa upande mwingine, Mahakama imemuachia huru William Haji aliyekuwa mkaguzi mkuu wa hesabu za ATCL