Jumanne , 23rd Mei , 2017

Aliyekuwa mshauri wa Chama cha ACT Wazalendo, Albert Msando amejiuzulu nafasi yake hiyo kufuatia video chafu zilizomuhushisha kuvuja kwenye mitandao ya kijamii hivyo ameamua kujiuzulu ili kuwajibika na kuomba radhi kwa wananchi kwa kitendo hicho

Wakili Alberto Msando

Kiongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe, amethibitisha kupokea kwa barua hiyo na kukubaliana na kiongozi huyo kwa kitendo chake hicho cha kuwajibika kisiasa huku akieleza kuwa, Bw. Msando amekuwa na mchango mkubwa katika Chama chao. 

"Nimepokea barua ya Wakili Albert G. Msando kuomba kujiuzulu nafasi yake ya Ushauri wa Chama chetu cha ACT Wazalendo. Ndugu Msando anawajibika Kwani anapaswa, nanukuu kutoka katika barua yake, "kuishi Kama mfano Kwa jamii inayonizunguka". Ndugu Albert Msando amekuwa kiongozi mwenye mchango mkubwa katika chama katika nafasi mbalimbali alizoshika ndani ya chama. Chama kinamshukuru kwa moyo wake wa uzalendo na mchango alioutoa katika Chama. Ni matumaini yetu ataendelea kushirikiana nasi katika ujenzi wa chama kwa kadri atakavyoweza na atakapohitajika kama mwanachama"- alisema Zitto Kabwe.

Zitto Kabwe pia ametumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi wamsaidie katika jambo hilo analopitia saizi 

"Nikiwa Kiongozi wa Chama nimekubali kuwajibika kwake na kumtakia kheri katika kujisahihisha kwake. Ndugu Msando Alberto ameomba msamaha Kwa jamii kwa uwazi na ni wajibu wetu kumsaidia kupita katika mitihani iliyomkumba" alimaliza Zitto Kabwe.