Jumanne , 28th Jun , 2022

Tanda Thadeo ambaye ni mkazi wa Sumbawanga mkoani Rukwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kuwatumia wanafunzi wa Darasa la sita shule ya msingi Kasisiwe iliyopo Manispaa ya Sumbawanga kushiriki zoezi la kufukua kaburi la mtoto  ili afufuliwe na baba yake kwa  kuwalipa  shilingi elfu kumi

Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani Rukwa ACP Theopita Mallya

Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani Rukwa ACP Theopita Mallya amethibitisha kuwa jeshi hilo linamshikilia Tanda Thadeo mwenye miaka 30 mkazi wa kitongoji cha Kasisiwe kilichopo manispaa ya Sumbawanga kwa tuhuma za kuwatumia wanafunzi hao kwa madai ya kumfufua mwanae hali ambayo imempelekea Kamanda wa Jeshi la  Polisi mkoa wa Rukwa kuitembelea shule hiyo na kutoa elimu kwa wanafunzi ya kutambua matendo ya kihalifu.

Hata hivyo Marry Kway  ambaye ni kamanda wa Jeshi la Polisi wilaya ya Sumbawanga naye alikuwepo kwa ajili ya kutoa somo la ukatili wa kijinsia na namna ya kuripoti matukio ya kiharifu kwa wanafunzi wa shule hiyo ili kupunguza vitendo vya uvunjifu wa amani kwa jamii.


Mtoto huyo aliefariki mwenye umri wa miaka  miwili alijulikana kwa jina la Martine Tanda na alizikwa 17.6.2022 kidini kwenye makaburi ya kitongoji cha Kasisiwe.