Jumamosi , 23rd Sep , 2017

Mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero huenda akaweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa klabu hiyo endapo atafunga ‘Hat trick’ leo kwenye mchezo wa EPL dhidi ya Crystal Palace.

Nyota huyo wa Argentina kwasasa ana mabao 175 ikiwa ni mawili nyuma ya Erick Brook ambaye anashikilia rekodi ya ufungaji bora ndani ya klabu hiyo akiwa na mabao 177.

Kocha wa Man City Pep Guardiola amemtaka mshambuiaji huyo kucheza bila presha ya kufunga mabao huku akishirikiana na wenzake na suala la kufunga kwake litakuja tu timu ikicheza kwa ushirikiano.

Aguero ameanza vizuri msimu wa 2017/18 ambapo hadi sasa amefunga mabao 5 na leo yupo fiti kuivaa Crystal Palace kwenye mchezo utakaoanza saa 11:00 jioni.