Jumatatu , 30th Nov , 2020

Mbunge wa Jimbo la Ilemela Dkt Angeline Mabula ametoa rai kwa wazee kukemea mmomonyoko wa maadili na vitendo visivyo vya kufaa ilikujenga jamii yenye usawa na yenye maendeleo.

Mbunge wa Jimbo la Ilemela Dkt Angeline Mabula

Dkt. Mbaula ametoa rai hiyo wakati akizungumza na wazee jimbo hilo ambapo amewashukuru kwamchango katika kufanikisha ushindi wa chama cha Mapinduzi huku akiwasisitizia kukemea vitendo viovu vinavyofanywa na vijana kupitia mgongo wa siasa.

“Tukikaa kimya watoto wetu wataharibika, lazima tuchukue nafasi yetu katika kuonya, kukosoa, zamani ilikuwa ukikosea mzee yeyote anakuonya anakuchapa au kukusema bila kujali wewe ni mtoto wake wa kuzaa au la “ amesema Dkt. Mbaula

Kwa upande wa wazee katika jimbo hilo wameahidi kuendelea kupambana na vitendo vinaleta mmomonyoko wa maadili kwa vijana na kuchukua hatua ili kuvitokomeza

Aidha Dkt Mabula amewahimiza wazee katika jimbo hilo kuendelea kushirikiana pamoja katika kuhakikisha wanaleta maendeleo ndani ya jimbo na taifa la Tanzania kiujumla.