Jumanne , 18th Aug , 2020

Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), imeanzisha mfumo mpya wa uwasilishaji wa fomu ya mlipa kodi kwa njia ya kielektroniki, ambapo mfumo huo pia unamtaka kila mfanyakazi ambaye anakatwa kodi ya mshahara kuwa na TIN Namba.  

Afisa Mwandamizi wa Kodi kutoka TRA, Isihaka Sharifu.

Hayo yamebainishwa hii leo Agosti 18, 2020 na Afisa Mwandamizi wa Kodi kutoka TRA Isihaka Sharifu, wakati wa mahojiano maalumu na SupaBreakfast ya East Africa Radio  walipotembelea Makao Makuu ya TRA Dar es Salaam.

"Wafanyakazi wote ambao wanakwatwa kodi ya Mashahara PAYE ni lazima kuwa na TIN,  hii ni katika Mfumo huu mpya", amesena Isihaka.