Jumatano , 21st Sep , 2022

Wafanyabiashara wa mbao mkoani Njombe wamesema wanakwama kufanya biashara hiyo kwa sababu ya mlundikano wa kodi na ushuru unaosababishwa nabaadhi ya maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TRA ) na halmashauri ya wilaya hiyo.

Mbao zikiwa sokoni

Wakizungumza katika kikao cha wafanyabiashara wa mbao na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Bw.  Anthony Mtaka chenye lengo la kuangalia changamoto za biashara hiyo.

Wafanyabiashara wamepata fursa ya kuwasilisha changamoto zao ikiwemo kodi ya Ongezeko la thamani VAT sambamba na kodi zingine zinazogusa biashara hiyo ambayo imeajiri watu wengi katika mkoa huo wa Nyanda za juu kusini.

Ushuru wa mageti unaokusanywa na halmashauri za mkoa huo nao umetajwa kuwa miongoni mwa changamoto hizo kwa wafanyabiashra hao, huku Suala la usajiri wa vibali vya Wakala wa Misitu Nchini (TFS) likiombwa kufanyiwa marekebisho, ambapo Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka akiwataka wafanyabishara kuwa huru kuwasilisha malalamiko yao ili serikali iyafanyie kazi.