Alhamisi , 24th Sep , 2020

Mamlaka ya Mapato nchini imewataka wananchi kuendeleza utaratibu wa kulipa Kodi mbalimbali kwa wakati huu ambao mamlaka hiyo huendelea na utaratibu wa kuanzisha vituo vipya vya huduma za kikodi kwa mlipa kodi.

Mkurugenzi wa Elimu kwa mlipakodi TRA Richard Kayombo

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Elimu kwa mlipakodi Richard Kayombo mara baada ya kutembelea kituo kipya cha huduma za kikodi kilichoanzishwa eneo la Chanika jijini Dar es salaam akieleza kwa sasa huduma mbalimbali zitapatikana hapo huu ukiwa ni mikakati wa Mamlaka hiyo kusogeza huduma karibu zaidi kwa wananchi.

"Kuanzishwa kwa kituo hiki cha huduma za kikodi hapa Chanika itawasaidia wafanyabiashara wengi kupata huduma kirahisi zaidi tofauti na umbali mrefu uliokuwa ukiwakabili TRA ni yenu msisite kuzitembelea ofisi hizi na kuuliza huduma yoyote"-Richard Kayombo.

Kwa upande wao wafanyabiashara Katika eneo hilo la Chanika wamesema wamekuwa wakipata changamoto ya kutembea umbali mrefu kutafuta huduma za kikodi hali ambayo wengi walitumia pia mwanya huo kukwepa ulipaji wa kodi stahiki kwa wakati.