Jumatatu , 26th Sep , 2022

Wakati raia wakiendelea kulalama juu ya kuzidi kuongezeka kwa bei ya nafaka ikiwemo mahindi kwa ajili ya unga.

Magunia ya mahindi

Ripoti ya mapitio ya uchumi ya mwezi Agosti, 2022 yaani (Monthly Economic Review) iliyotolewa na benki kuu ya Tanzania (BoT) inaeleza kuwa bei ya jumla ya gunia la Kilo 100 la mahindi kwa mwaka ulioishia Julai 2022 ilikuwa Sh. 87,383 kutoka Sh. 43,371 iliyorekodiwa kipindi kama hicho mwaka jana. 

"kwasasa mahindi ni kweli yamepanda sana bei, kilo moja ni zaidi ya shilingi 1000 wakati mwaka jana ilikuwa 500 bei ya juu. sababu hapa ni kufunguliwa kwa mipaka kwasababu walivyoruhusu tu mipaka kupitisha mahindi watu wa nje wakaja kununua na wale wakija kununua wao wananaunua kwa bei yoyote na hii ikapelekea mahindi kupungua kwanza nchini, lakin i pia wafanyabiashara wakalazimika kununua kwa bei kubwa kutoka kwa wakulima kwasababu bila kufanya hivyo tusingepata kitu, kingine ni bei ya kusafirisha ambapo sasahivi tunatumia hadi milioni mbili kuleta mzigo mjini tofauti na mwaka jana ambapo milioni moja ilikuwa inatosha kwenye usafiri" - Khatibu Kiroboto, Mfanyabiashara wa mahindi Tandare.

Hivyo basi, hiyo ni sawa na kusema kwamba, wakulima na wafanyabiashara wa mahindi wametia kibindoni Sh. 44,012 zaidi kwa kila gunia moja au sawa na kusema bei hiyo ya mahindi imeongezeka zaidi ya mara mbili ikilinganishwa na bei ya mwaka jana.